Shinda na SIM Account

Picha: Pogba na Jesse Lingard wakimnywesha mtoto wa Chui maziwa

Mastaa wa Manchester United, Paul Pogba na Jesse Lingard wameonekana wakitumia muda wao mwingi kumpatia lishe ya maziwa mtoto wa Chui mwenye asili ya rangi nyeupe siku ya Alhamisi wakati timu hiyo ikiwa katika maandalizi ya msimu katika Falme za kiarabu huko Dubai kitendo ambacho kimevuta hisia za wadau wengi wasoka.

 

Lingard ameweka kipande cha video katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram kikiwa kinaonyesha namna kiungo huyo anavyocheza na mtoto huyo wa Chui huku akimpatia maziwa kupitia chupa.

Wakati, Pogba naye ameonekana akimpatia maziwa mtoto huyo wa Chui huku akimbusu katika kichwa chake.

Meneja, Jose Mourinho sasa amemaliza maandalizi yake Dubai na mapumziko yao baada ya kupita kipindi kigumu cha msimu wa ligi ya England.

Kikosi cha United kinatarajia kurejea siku ya Jumatatu ambapo kitakuwa na kibarua cha kuwakabili Stoke katika dimba la Old Trafford.

Mpaka sasa wapenzi wa soka wanahamu ya kutaka kufahamu kama Mourinho atafanya usajili katika dirisha hili la mwezi Januari.

Habari amabazo zimeenea ni kwamba Mreno huyo yupo katika ushindani na Manchester City wa kuwania saini ya mchezaji wa Arsenal, Alexis Sanchez.

Viongozi wa ligi ya England, Man City wametoa ofa ya paundi milioni 20 kwa  Sanchez, wakati wapinzani wao United wakitoa 250,000  huku Arsenal wakihitaji  paundi milioni 35.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW