Picha: Prince Harry na Meghan Markle wawatembelea watoto wa shule Birmingham kwenye Siku ya Wanawake Duniani

Katika ksherehekea siku ya wanawake duniani, Prince Harry na mpenzi wake Meghan Markle wametembelea katika mji wa Birmingham na kukutana na wanafunzi wadogo wa shule.

Miongoni mwa wanafunizi hao wadogo ambao wamekutana nao ni Sophia Richards Oasis Academy Warndon ambaye alimueleza Harry na Meghan kuhusu ndoto zake za hapo baadae.

Sofia aliwaambia wawili hao kuwa ndoto zake ni kuwa muigizaji mkubwa. Hata hivyo Prince Harry alimjibu mtoto huyo kwa kumwambia, “Unahitaji kuwa na uhakika na unaweza kufikia chochote unachotaka kufikia.”

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW