Shinda na SIM Account

Picha: Rais Mugabe aonekana kwa mara ya kwanza hadharani

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza leo tangu siku ya Jumatano alipokuwa amehifadhiwa na jeshi la nchi hiyo sehemu isiyofahamika.


Rais Robert Mugabe akihutubia katika sherehe za Chuo Kikuu mjini Harare Ijumaa hii

Mugabe alihudhuria katika sherehe za kuhitimu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu mjini Harare.

Kwa taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Zimbabwe zinadai, Rais Mugabe alishangiliwa sana baada ya kumaliza kuhutubia katika sherehe hizo.

Kiongozi huyo wa Zimbabwe aliibua mzozo mzito tangu alipotangaza kumfuta kazi Makamu wake wa Urais, Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita kwa madai amekuwa sio mzalendo wa nchi yake na nafasi. Baada ya hatua hiyo maneno yalianza kuibuka kuwa Mugabe anamtengenezea njia nzuri mkewe Grace Mugabe kuja kurithi kiti chake cha Urais.

Japo Mugabe ameonekana kuwa chini ya usimamizi wa jeshi lakini amedaiwa kukataa wito unaomtaka ajiuzulu kwa hiari yake.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW