Habari

Picha: RC Makonda alivyofanya ziara yake ya kwanza Zanzibar

Jumatatu hii Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefanya ziara yake ya kwanza ya kujifunza katika kisiwa cha Unguja kwa kutembelea sehemu mbalimbali za utalii wa kisiwa hiko na baadhi ya miradi ya maendeleo.

Katika ziara ya kiongozi huyo alikuwa ameongozana na mwenyeji wake amble pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud. Baadhi ya sehemu ambazo Makonda ametembelea ni pamoja na Pango la Tumekuja, Kanisa la Mkunazini, Jumba la Treni, Hotel ya Mtoni Marine, Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ), Nyamanzi, Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe, Kiwanda cha Sukari Mahonda na shamba la Spice Tour Kizimbani.

Hizi ni baadhi ya picha za ziara hiyo.


Mhe. Makonda akisaini kitabu chaa wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi


Mhe. Makonda na Ayoub wakiwa katika picha ya pamoja katika kanisa la Mkunazini


RC Makonda na Ayoub wakiwa katika hoteli ya Mtoni Marine inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu Bakhresa


Makonda na Ayoub wakiongea na wananchi wa eneo la soko la Darajani

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents