Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Picha: Rihanna akava jarida la Vogue Paris la mwezi Disemba

Rihanna anazidi kupata tobo katika tasnia ya mitindo. Msanii huyo baada ya kutokea kwenye jarida la Vogue Arabia, amepata shavu jingine la kukava jarida la Vogue Paris.


Kava ya kwanza ya jarida la Vogue Paris, Rihanna akiwa amevalia nguo za Juergen Teller wa Ujerumani

Katika jarida hilo ambalo linatarajiwa kutoka mwezi Disemba mwaka huu kama zawadi ya sikukuu ya Christmas, mrembo huyo ametupia mavazi ya wabunifu watatu maarufu duiani akiwemo Jean-Paul Goude, Juergen Teller and Inez & Vinoodh.


Kava ya pili ya Vogue Paris, Rihanna akiwa amevalia nguo za Inez & Vinoodh wa Uholanzi

Jarida hilo linatarajiwa kuwa na kava tatu tofauti ambazo Rihanna ataonekana. Katika kava ya kwanza mrembo hyo ametupia mavazi ya mbunifu Juergen Teller wa Ujerumani, wakati kava ya pili ametumia mavazi ya Inez & Vinoodh wa Uholanzi.


Kava ya tatu ya jarida la Vogue Paris ambapo Rihanna amevalia nguo za Jean-Paul Goude kutoka Ufaransa

Katika kava ya mwisho Riri amepigilia mavazi ya Jean-Paul Goude kutoka Ufaransa.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW