Burudani

Picha: Rob Kardashian na Black Chyna waifunga midomo ya wanafiki

By  | 

Baada ya uvumi kuzagaa kwa muda mrefu kuwa Rob Kardashian na Black Chyna, wametengana, hatimaye wawili hao wamewafunga midomo wanafiki kwa kudhihirisha wapo pamoja, tena sana tu.

Wawili hao wamethihirisha hilo siku ya jana katika siku ya baba duniani walipokuwa kwenye mji wa Disneyland kusherekea siku hiyo na mtoto wao wakike Dream mwenye miezi saba pamoja na mtoto wa Black aitwaye, King Cairo.

Rob na Black walihisiwa kutengana tangu Februari mwaka huu baada ya Rob kuonekana akihama katika nyumba aliyokuwa akiishi na Black, ila inadaiwa kuwa moja ya chanzo kilicho zua ugomvi kati yao ni Black alimtaka mzazi mwenzake huyo ajipunguze mwili lakini hali likuwa ngumu kwa upande wa kijana huyo kutoka familia ya Kardashian kwani alishindwa kabisa kupungua, hivyo Black akaona isiwe tabu ngoja nikuache kidogo.

Hata hivyo inasadikika kuwa Black hakuachana na mzazi mwenzake huyo ila alikuwa akitafuta attenshion za watu katika mitandao ya kijamii.

Na Laila Sued

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments