Michezo

Picha: Robinho aanza mazoezi na timu yake mpya Uturuki

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid na Masnchester City, Robinho ameanza rasmi mazoezi na timu yake mpya ya Sivasspor inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uturuki.

Robinho amejiunga na timu hiyo kama mchezaji huru akitokea klabu ya Atlético Mineiro ya nchini kwao Brazil ambayo ameichezea kwa msimu mmoja.

Mwezi Novemba mwaka jana mchezaji huyo alihukumiwa kifungo cha miaka jela nchini Italia kutokana na kosa la ubakaji alilomfanyia mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 23 huko mjini Milan mwaka 2013.

Hata hivyo mchezaji huyo alikata rufaa ambayo inadaiwa kuwa inaweza kuchukuwa mwaka mmoja rufaa hiyo kukamilika huku akiruhusiwa kuendelea na kazi yake ya kucheza mpira.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents