Burudani

Picha: Run Down ya Fainali za Miss Ilala 2012

Jana Usiku ilikua fainali ya Miss Ilala ambapo taji hilo lilikuwa likishikiliwa na Salha Israel, ambaye ndiye Miss Tanzania.

Salha alimkabidhi taji mrembo mpya wa kuiwakilisha Ilala katika mashindano ya taifa mwaka huu.

Taji hilo lilienda kwa Noela Malik,na mlimbwende Madgalena Roy Munis akiwa wa pili huku wa tatu akiwa Mary Chizi ambaye pia alikua mshindi wa Talent.

Burudani mbalimbali kutoka kwa Banana Zorro na The B-Band pamoja na Chege zilikuwepo, pamoja na kutoka kwa vikundi vingine vingi.

Mgeni rasmi alikuwa meya wa Ilala,Mh. Jery Slaa huku show ikiongozwa na Steve Nyerere pamoja na Gadna G Habash ambaye pia alikua kati ya waandaaji wa shindano hilo.

Washiriki walikuwepo kumi na tano na hawa walio fanikiwa kuingia tano bora walikua ifuatavyo;

mrembo namba 7-Noela Maliki
mrembo namba 3-Madgalena Roy Munis
mrembo namba 8-Elizabet Kyelo
mrembo namba 6-Matilda Martini
mrembo namba 13-Mary Chizi

Cheki Shughuli nzima ilivyoenda,

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents