Burudani

Picha: Selena Gomez na Justin Bieber wathibitisha ni wapenzi

By  | 

Bado huamini kama Selena Gomez na Justin Bieber kama wamerudiana? Basi unatakiwa kuaamini hilo.

Jumatano hii wawili hao wameonekana wakidendeka huko mjini Los Angeles katika uwanja wa kuteleza wa barafu ambao unatumika kuchezea mpira wa magongo ambapo Bieber alikuwa ni mmoja wa wachezaji wa mchezo huo.

Selena na Bieber walianza kuonekana wakiwa pamoja mapema mwezi huu baada ya kusambaa kwa taarifa za Selena kuachana na aliyekuwa mpenzi wake The Weeknd.

Selena na Justin waliwahi kuwa wapenzi kwa miaka mingi kabla ya kuachana na kurudiana tena hivi karibuni.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments