Michezo

Picha: Serena Williams akava jarida la Vanity Fair akiwa mtupu na ujauzito wake

Mastaa wakubwa duniani hasa wakike wamekuwa wakitumia picha zao za utupu kuendelea kukaa midomoni mwa mashabiki. Tumezoea kuwaona kina Kim Kardashian, Nicki Minaj, Amber Rose na wengine wakifanya hivyo, lakini sasa ni zamu ya Serena Williams.

Bingwa huyo wa mchezo wa tennis katika mashindano ya Australian Open, amewashtua mashabiki baada ya kupiga picha za jarida la Vanity Fair akiwa mtupu na ujauzito wake wa miezi sita.

Serena anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza mwaka huu na mchumba wake Alexis Ohanian. Katika jarida hilo Williams amefunguka kuwa atarejea tena uwanjani mwezi January mwakani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents