Habari

Picha: Siku ya mwisho ya kuuga mwili wa Mandela, watu 100,000 wajitokeza, wengine waumia wakigombania kumuaga

Jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa wananchi wa Afrika Kusini na wageni kutoa heshima zao za mwisho kwa Rais wa zamani wa taifa hilo Nelson Mandela, baada ya kutengwa siku tatu kwaajili ya zoezi la kuuaga mwili wake uliowekwa katika ofisi za serikali jijini Pretoria.

LD-2
Watu waliojipanga mitaani wakati mwili ukipelekwa Union Buildings kuagwa siku ya mwisho

Ripoti zinasema umati mkubwa ulijitokeza katika siku hizo tatu, na misululu ya watu wapatao laki moja ilijipanga kwa umbali mrefu wakisubiri kumuaga shujaa wao jana huku wengine wakiambulia kuuona tu katika gari.

ld-1
Polisi wakijaribu kuwazuia watu wasiendelee kuingia

Kutokana na umati mkubwa uliojitokeza, polisi walijaribu kuzuia watu wasiendelee kuingia kwa kufunga mageti, lakini hata hivyo watu hao walilisukuma na kutaka kuingia kwa nguvu ili na wao wakatoe heshima zao za mwisho.

LD-10

Katika vurugu hizo baadhi ya waombolezaji walianguka na kukanyagana, baadhi yao walipata majeraha madogo.

LD-3

LD-4

LD-5

LD-6

Huko kijijini Qunu ambako mwili wa Mandela unatarajiwa kupelekwa leo tayari kwa mazishi yatakayofayika kesho Jumapili, maandalizi yako katika hatua za mwisho.

LD-12
Qunu, maandalizi ya mwisho yakifanywa tayari kupokea mwili kwa mazishi kesho

LD-11

Siku ya Jumatatu (December 16) baada ya mazishi, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajiwa kuzindua sanamu ya Nelson Mandela, ambayo imeonekana ikimaliziwa kuwekwa katika ofisi za Serikali ‘Union Buiildings’ jijini Pretoria jana.

LD-9
Sanamu ya Mandela ikimaliziwa

LD-8

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents