Burudani ya Michezo Live

Picha: Tamasha la funga mwaka lilivyofanyika Escape One

Usiku wa Ijumaa ya Disemba 30 kulikuwa na show ya kuufunga mwaka wa 2016 iliyofanyika katika ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.


Anton ambaye alikuwa mshereheshaji wa shoo hiyo akiwatambulisha wahitumu wapya wa Muziki kutoka THT.

Tamasha hilo lilifunguliwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mhe. Ally Hapi huku wasanii kibao waliwasha moto kwenye tamasha hilo akiwemo Bushoke, Maua Sama, Barnaba, Belle9, Ditto, Mwasiti, Nandy, Hamadai, wasanii wengine ambao walitoa show ni Nuh Mziwanda, Nedy Music na Lulu Diva.


Mheshimiwa Ally Hapi akitoa salam kwa wageni walio fika katika show hiyo.


Sebastian Ndege akimtunza msanii Lameck Ditto wakati akiimba wimbo wake ambao unafanya vizuri kwa sasa wa Moyo Sukuma Damu


Bushoke na Maua Sama wakiimba jukwaani wimbo wao mpya unaitwa Tupendane Sasa.


Msanii Bell9 akitoa burudani


Wasanii Barnaba na Nandy wakitoa burudani


Msanii Lulu Diva


Bushoke akitoa burudani

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW