Habari

Picha: Umoja Cultural Flying Carpet – Makumbusho, Dar es Salaam

Umoja Cultural Flying Carpet ni mpango uliobuniwa kwaajili ya kupromote amani na maendeleo katika jamii kupitia shughuli za kitamaduni zinazoshirikisha mataifa mbalimbali.

Mwaka huu maonesho hayo ya tamaduni yanafanyika jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Makumbusho ambapo kuna vikundi vya sanaa kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia na Norway ambao ndio wadhamini wakubwa wa maonesho hayo.

Jana Jumapili kulikuwa na show za utangulizi ambapo wasanii kutoka Norway, Uganda, Kenya, Tanzania na Ethiopia walitumbuiza.

Pamoja na burudani ya muziki, tamasha hilo lilipambwa na onesho safi la sarakasi kutoka kwa wasanii wa Ethiopia waliozikonga vyema nyoyo za watu waliohudhuria.

October 5 mwaka huu kutafanyika onesho rasmi kuanzia saa 1 na nusu jioni katika viwanja vya Makumbusho, Dar es Salaam.

Hizi ni baadhi ya picha za tukio la jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents