Michezo

Picha: United yaongoza maelfu ya mashabiki kumbukumbu ya ajali ya ndege

Klabu ya Manchester United imeongoza maelfu ya mashabiki kutoa heshima zao katika kumbukumbu ya watu 23 waliyofariki dunia kufuatia ajali ya ndege iliyotokea huko Munich miaka 60 iliyopita.

Meneja wa timu hiyo, Jose Mourinho pamoja na wachezaji wake walikuwepo  katika viunga hivyo huku legendari wa Old Trafford, Sir Bobby Charlton ambaye alinusurika katika ajali hiyo ya Februari 6 mwaka 1958 akiwa ni miongoni mwa waliyohudhuria kwenye kumbu kumbu hiyo  akiwa sambamba na Sir Alex Ferguson.

Katika kumbu kumbu hiyo iliongozwa na kukaa kimya kwa muda na kuimba mashahiri mbalimbali.

Picha zikiwaonyesha wachezaji wa Man United, mashabiki na baadhi ya waliyo wahikuihudumia timu hiyo 

Wachezaji wa kikosi kilichopata ajali picha hii ikiwa ni kabla ya tukio hilo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents