Burudani

Picha: Vanessa Mdee aingia studio kurekodi ngoma na rapper Tay Grin wa Malawi

Vanessa Mdee alitumbuiza kwenye show ya mkesha wa mwaka mpya nchini Malawi, mwishoni mwa wiki. Lakini hakuishia tu kutumbuiza, bali alitumia muda huo kurekodi wimbo anaoshirikishwa na rapper wa nchini humo, Tay Grin.

Vanessa Mdee akiingiza sauti kwenye booth

Kwa muda mrefu Tay alikuwa akidai kuwa anapenda aje arekodi wimbo na muimbaji huyo wa Cash Madame, na sasa fursa hiyo imepatikana hatimaye.

Vee na Tay wameshare picha kadhaa za studio session yao kwenye Instagram.

“Studio session! @vanessamdee @sonyezo and yours truly. The fire levels on this song is on the higher side. CANT wait for y’all to hear it. Too much ????????????????,” ameandik Tay.

Vanessa Mdee akiwa amejilaza kwenye kochi wakati Tay Grin akiingiza sauti zake

Mwaka jana Tay aliiambia Bongo5: Napenda jinsi wasanii wa Tanzania wanavyoimba. Ni kimuziki sana hata kama sizungumzii Kiswahili, muziki wao unasikika vizuri na ni mtamu. Nimesikiliza wasanii kama Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Alikiba na muziki wao wa Bongo Flava. Nadhani Nyau Music inaweza kuchanganyikana vizuri na wasanii hawa wakali. Kwa sasa ninafanyia kazi wimbo na Vanessa Mdee na nina matumani ya kumpata Diamond Platnumz kwenye wimbo huo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents