AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Picha/Video: Rick Ross atua Kenya, kuwasha moto kesho

Rick Ross tayari ametua ndani ya Kenya kwa ajili ya kufanya show yake ya kufa mtu April 28 ya mwaka huu.

Bosi huyo wa Maybach Music Group, amepokelewa kwa shangwe kubwa kwenye uwanja wa ndege wa nchini humo ikiwa ni mara yake ya pili kutia Afrika Mashariki baada ya kutua Bongo kwenye tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam Oktoba mwaka 2012.

Baada ya kutua Ross amesema anafuraha kubwa kutua Kenya. Tamasha hilo ambalo limeandaliwa na kituo cha radio cha NRG Radio, linatarajiwa kufanyika kenye ukumbi wa hiyo kwenye ukumbi wa Carnivore uliopo mjini Nairobi.

Rick Ross anatarajiwa kupanda jukwaani na wasanii wengine wa Kenya akiwemo Khaligraph Jones na Nyashinski kutoka Kenya.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW