DStv Inogilee!

Picha/Video: Vanessa, Jux walipowatembelea watoto Muhimbili na kuimba nao

Msanii wa muziki Bongo, Vanessa Mdee na mpenzi wake, Jux wamewatembelea watoto wanaotibiwa saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Vanessa ameeleza lengo la kufanya hivyo ni kuijulisha jamaii kuwa selikali inatoa matibabu ya saratani bure kwa watoto wote Tanzania na pia waelewe kuwa saratani ya watoto inatibika. Kupitia ukurasa wa Instagram Vanessa ameandika;

“Imekuwa siku nzuri ya furaha na baraka tele, nilipata fursa ya kuwatembelea wadogo zangu wanaotibiwa saratani Muhimbili. Tumecheza na kuimba na pia tumekata keki,” ameeleza Vanessa.

Nchi ya Tanzania inakadiriwa kuwa na watoto 4,500 wenye Saratani kwa kila mwaka, katika idadi hiyo ni asilimia 20 tu ndio wanafika hospitali kupata matibabu.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW