Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Picha & Video: Waziri Kairuki akabidhi ofisi kwa waziri mpya

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amekabidhi ofisi kwa Waziri mpya wa Utumishi, George Nkuchika huku akimueleza kuwa changamoto ya uhakiki wa vyeti hatoisahau katika wizara hiyo.

Waziri Kairuki ameyasema hayo leo alipokuwa akifanya makabidhiano hayo kwa Waziri huyo baada ya Baraza la Mawaziri kufanyiwa mabadiliko na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Hata hivyo Waziri Kairuki amesema kuwa wakati wa uhakiki kuna baadhi ya watendaji alioshirikiana nao hawakuwa waaminifu hivyo walijipenyeza na watu wasio na sifa.

Kwa upande wake, Waziri Mkuchika amesema kuwa atayaendeleza aliyoyaacha  ikiwemo kudumisha nidhamu katika utumishi wa umma na kupiga vita rushwa.

Oktoba 7 mwaka huu, Rais Magufuli alifanya Mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo baadhi ya mawaziri wamepoteza nafasi zao huku baadhi wakipanda na wengine wapya wakiteuliwa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW