Habari

Picha: Waandishi Mexico wafanya maandamano kupinga mauaji ya mwenzao

By  | 

Jumanne hii yamefanyika maandamano makubwa nchini Mexico wakipinga mauaji ya mwandishi Javier Valdez ambaye alipigwa risasi na kufariki mjini Sinaloa.

Mwandishi huyo alifanikiwa kujizolea tuzo mbalimbali kutokana na ujasiri wake wa kutoa taarifa za kufichua magenge ya wauzaji wa madawa ya kulevya nchini humo.


Picha ya Javier Valdez enzi za uhai wake

Imedaiwa kuwa waandishi wa habari katika mji wa Mexico City wameandika barua katika ofisi ya mwanasheria mkuu wa nchi hiyo wakiomba wapatiwe ulinzi zaidi na haki iweze kutendeka kwa waandishi wengine watano ambao wamefariki kwa kuuawa tangu mwaka huu ulipoanza.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments