Picha: Wamarekani waingia mtaani kuandamana baada ya muuaji wa Trayvon Martin, George Zimmerman kuachiwa huru
Rais wa Marekani, Barack Obama jana amelazimika kuomba hali ya utulivu nchini humo kufuatia kuachiwa huru kwa George Zimmerman anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi kijana mwenye asili ya Afrika, Trayvon Martin.
Mwanamke akilia kwa uchungu
Vilio na maandamano
Katika maelezo yake, Obama alikiita kifo cha Martin kama janga la Marekani lakini alisisitiza “sisi ni taifa la sheria, na majaji wamezungumza.”
“Namuomba kila Mmarekani kuheshimu wito wa utulivu uliotolewa na wazazi wawili waliompoteza kijana wao mdogo,”alisema.
Kundi la watu maalum mahakamani (jury) jimboni Florida nchini humo, Jumamosi usiku liliamua kuwa Zimmerman, aliyekuwa kwenye zamu ya kulinda usalama katika maeneo anayoishi, kuwa hana hatia kwa kosa la mauaji ya Martin, 17, aliyekuwa akipita usiku huo February mwaka jana.
Kesi hiyo ilikuwa imechukua hisia za watu wengi nchini Marekani na ilikuwa ikihusisha suala la ubaguzi wa ragni. Kutokana na kesi hiyo, maelfu ya watu nchini kote wameingia mtaani kupinga hukumu hiyo na wengine walikusanyika nje ya Ikulu ya Marekani.
Maandamano bado yanaendelea na huenda kesi hiyo ikaangaliwa tena.
Picha zaidi: