Habari

Picha: Wananchi wa Venezuela wamkalia kooni Rais Nicolas Maduro

Maandamano ya kumpinga Rais Nicolas Maduro wa Venezuela, yameingia katika siku ya pili nchini humo katika mji mkuu wa Caracas.

Maelfu ya raia wa nchi hiyo wameendelea kuandamana wakiongozwa na viongozi wa vyama vya upinzani, huku wakimtaka rais huyo kuachia madaraka, kutokana na mwenendo mbaya wa kiuchumi unasimamiwa na serikali yake.

Mmoja wa waandamanaji hao ambaye alitambulika kwa jina la Sandra Vanessa, ameiambia Al Jazeera kwamba “Pamoja vurugu zinazoendelea nchini lakini wito huu ni muhimu. Tunapigania haki zetu, tunakabiliwa na uhaba wa chakula, kuna umasikini na watu wetu wanakufa katika hospitali. Hatuwezi kupata antibiotics. Hivyo ni muhimu kuandamana.

Hadi siku ya Jumatano watu watatu walifariki dunia katika maandamano hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents