Tia Kitu. Pata Vituuz!

Picha: Wananchi wakiwa na shauku ya kuwaona wapenzi waliogandana wakati wa tendo

Haikuwa rahisi kwa wananchi waliokuwa wamefurika kwenye hospitali ya wilaya ya Temeke, kuamini maneno ya walinzi na mganga mkuu wa hospitali hiyo kuwa wapenzi wanaodaiwa kugandana wakati wa tendo la ndo hawakuwepo ndani ya hospitali hiyo.

Habari zilidai kuwa mwanaume mmoja alitembea na mke wa mtu ambaye alikuwa amewekewa tego na mume wake kiasi cha kushindwana kuachiana mara baada ya kufanya mapenzi.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo hospitalini hapo, walidai kuwa watu hao waliingizwa kwenye hospitali hiyo wakiwa wamefunikwa shuka na kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ili kuepusha usumbufu katika wodi za wagonjwa.

Wengine walisema kuwa wakati wakiingia, mwanamke alikuwa mbele na mwanaume nyuma na kuwafanya watu waamini kuwa ndivyo walikuwa wakifanya tendo hilo.

Hata hivyo mganga mkuu wa hospitali hiyo alikanusha kupokea watu hao na kusema kuwa hizo ni taarifa za uzushi.

Watu wengi waliokuwa na shauku kubwa ya kuwaona watu hao walizipuuzia taarifa hizo na kuendelea kuamini kuwa watu wamefichwa hospitalini na hivyo kuendelea kusubiria bila kuchoka hadi usiku.

Hadi tunaondoka eneo hilo lililokuwa likilindwa na polisi hakukuwa na dalili za watu hao kutolewa.

Hizi ni baadhi ya picha zilizochukuliwa kwenye eneo hilo. Video zinafuata.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW