Tragedy

Picha: Wasichana 2 waliomwagiwa Tindikali Zanzibar wawasili kwao Uingereza, tukio latawala vyombo vya habari vya huko

Mama mwenye hasira wa mmoja wa wasichana wa Uingereza waliomwagiwa acid mjini Zanzibar ameungana na bintiye nchini humo baada ya leo kuwasili kwa ndege kwenye hospitali kwaajili ya matibabu.

£££-The-two-acid-attack-victims-2145123
Katie Gee, aliyefunikwa blanket, na rafiki yake Kirstie Trup wakiwasili kwenye hospitali ya Chelsea and Westminster nchini Uingereza kutibiwa majeraha yao

Mama huyo, Nicky Gee alionekana kushindwa kujizuia kulia baada ya kumuona binti yake Katie na rafiki yake Kirstie Trup wakishuka kwenye ambulance akiwa amefunikwa blanket.

£££-The-two-acid-attack-victims-2145124

Wasichana hao ambao wote wana miaka 18 walipelekwa kwenye hospitali ya Chelsea and Westminster kutibiwa haraka majeraha ambayo baba yake Katie ameyaita mabaya yasiyoelezeka.

article-2387651-1B381DE8000005DC-830_634x783

article-2387651-1B381EDA000005DC-119_634x520

Wote wameungua vibaya baada ya kumwagiwa tindikali usoni wakati walipokuwa wakiingia kwenye mgahawa mjini Zanzibar. Hilo lilikuwa shambulizi la tatu wakati walipokuwa visiwani humo. Awali mmoja wa wasichana hao alishambuliwa na msichana wa kiislam baada ya kumsika akiimba wimbo wakati wa mwezi wa Ramadhan.

Attachment-1
Katie baada ya kumwagiwa tindikali

article-2387651-1B383184000005DC-824_634x642

Last-picture-of-Kirstie-Trup-and-Katie-Gee-2140804
Katie na Kirstie

Polisi wamedai kuwa washukiwa saba akiwemo muongozaji wa watalii wamekamatwa jana asubuhi.Na sasa zawadi ya paundi £4,000 imetangazwa kutolewa na polisi Zanzibar kwa atakayesaidia kupatikana kwa kwa wahalifu hao.

Marafiki wanadai kuwa walikuwa wamelengwa kushambuliwa kwasababu walikuwa ni wayahudi na polisi wanadai kuwa walikuwa wanataka kuongea na mhubiri wa kiislam ambaye huenda ndiye alipanga shambulizi hilo.Polisi wamedai kutoa warrant ya kukamatwa kwa Sheikh Issa Ponda Issa, ambaye inasemekana mafundisho yake yamechochea mashambulizi hayo ya tindikali.

Wasichana hao watapata matibabu ya kina kutokana na mejeraha waliyoyapata kwa kumwagiwa tindikali hiyo iliyomwagika usoni, kifuani, miguuni na mgongoni.

article-2386666-1B3345C0000005DC-753_634x348
Katie

Mikono yao pia imejeruhiwa kwakuwa walikuwa wakijaribu kufuta tindikali hiyo. Baba yake na Miss Trup, Marc, 51, milionea na daktari wa meno alisema mpita njia alienda kuwasaidia wasichana hao baada ya kushambuliwa na alimpigia simu.

Marafiki hao walikuwa wameenda Zanzibar kama walimu wa kujitolea kwenye kituo cha watoto yatima.

Tukio hilo linaweza kuathiri vibaya sekta ya utalii visiwani Zanzibar.

“This does wonders for the tourism industry in Zanzibar, obviously they don’t need the money!! Hope the girls get thru this horrible incident,” ameandika msomaji mmoja kwenye mtandao wa Daily Mail.

‘Really wanted to book a holiday in Zanzibar, not anymore,’ ameandika mwingine aitwaye, Sassy1.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents