Habari

Picha: Watoto 44 wafariki katika maporomoko ya Colombia

Watoto takribani 44 wameripotiwa kufariki dunia mjini Mocoa nchini Colombia katika maporomoko yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha siku ya Jumamosi.

Rais wa nchi hiyo Juan Manuel Santos ametembelea eneo hilo kwa siku mbili na amesema zaidi ya watu 200 wamebainika kupoteza maisha huku katika ya hao watoto ni 44.

Wakati huo huo inadaiwa kuwa idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi kutokana na watu takriban 300 bado hawajulikani walipo. Mwanabaiolojia Carolina Pardo kutoka chuo kikuu cha El Rosario mjini Bogota,amezungumza na BBC akisema matumizi mabaya ya ardhi yamesababisha mmomonyoko wa udongo uliosababisha maporomoko ya ardhi.

Hii ni baadhi ya picha za maeneo yaliyoharibika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents