Burudani

Picha: Waziri Nape aendeleza operesheni ya kukamata CD za ujanja ujanja

Kwa mara nyingine Waziri Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye Ijumaa hii akiongozona na viongozi wa TRA, Basata, Cosota, Yona na Leseni wamefanikiwa kukamata shehena la CD feki huku nyingine zikiwa hazina nembo za TRA na wamefanikiwa kuwabaini baadhi ya wafanyabiashara wengine wakiwa hawana vibali vya kufanya biashara hiyo.


Waziri Nape akikatisha mitaa ya K/Koo kukagua maduka yanayouza CD

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo, waziri Nape amesema, “Operesheni hii ni ya kujaribu kuondoa kazi za sanaa na nyingi za kutoka nje ambazo kwanza hazijalipiwa kodi, hazijapata vibali na matokeo yake zinakuwa kazi zinazosambaa hapa nchini ambazo hazipitii katika vyombo vyetu na nyingi zipo chini ya kiwango na zingine zinafundisha vijana wetu maadili mabovu.”

“Wale tuliowakamata safari hii tutafuta leseni zao, kwasababu wameenda kinyume na leseni. Kwahiyo safari hii pamoja na kuzikamata zile mali na kuziharibu lakini pia lazima tuzifute leseni zao ili kama wanataka kufanya hii basi waombe upya leseni ili wafuate masharti yanayohusika. Sasa wale wote tutakaokuwa tumechukua kazi zao na tutakuwa tumechukuwa leseni zao tutakutana nao Jumatatu katika uwanja wa taifa.”

Naye mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Yono, Scholastica Kevela amesema, “Tumekuja mara kwa mara kuwakamata lakini bado wanaendelea. Sasa mimi kama Yona naingia kwenye utekelezaji na niseme tu hii awamu ya tano haina ‘mswalie mtume’, watu watii sheria bila shuruti na Yono tupo kazini tukikukamata na sisi hatuna masihara.”

Wakati huo huo mwakilishi kutoka TRA, amesema kuwa wamekuwa wakipoteza fedha nyingi sana za kodi kutokana na baadhi ya wafanyabishara hao kutofuata sheria iliyopangwa ya ulipaji kodi. Tazama picha zaidi za matukio hayo hapa chini.


Mfanyabiashara wa CD (kushoto mwanamke) akitoa maelezo kutokana na kosa la kuuza bidhaa zisizokuwa na stemp


Baadhi ya mizigo ya CD ikiwa tayari kwa kuchukuliwa kwenda kuteketezwa


Moja ya wafanyabiashara ya CD akiwa chini ya jeshi a polisi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents