Aisee DSTV!

Picha ya Gadner na mtoto wake yazua gumzo 

Picha ya Gadner na mtoto wake yazua gumzo 

Picha inayomuonyesha mtangazaji mahiri wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Gadner G Habash akiwa na mwanae Karen imezua gumzo kwenye mitandao kutokana na watu kutafsiri tofauti.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Gadner ameweka picha ambayo amerepost kutoka katika akaunti ya binti yake Karen ikiwa inaonyesha akiwa amemkumbatia mtoto wake  huku wakiwa wamelala kwenye kochi ndipo watu wakatafsiri kama watu ambao wapo kwenye mahusiano.
Lakini baada ya picha hiyo kwenda katika mitandao ya kijamii ilileta gumzo na kusemewa maneno mengi sana huku wadau na baadhi ya mashabiki wakisema kuwa hayo sio maadili ya kitanzania hasa kwa baba na binti yake.
Video ikimuonyesha baba Gadner akiwa na mwanae Karen wakipata chakula pamoja

Related Articles

99 Comments

 1. Yaani ukiwa baba utakiwi kugusa mwanao ema kukaa nae
  Acheni ujinga
  David Beckham alipokua na familia yake serengeti kamu kiss binti wake wengine povu liliwatoka tena
  Hamuna kosa hapo kwa sababu ukitazama iyo picture vizuri nikama walikua natizama tv mtoto kazidiwa na usingizi sijuwi baba kaja kamufukika na kukaa karibu yake
  Cha Kushangaza ni nini hapo

 2. Mambo mengine ni upuuzi,yaaani nisikae na mwanangu kisa maadili,yaaan mtoto nianze kum badilisha nepi akiwa mchanga,nimuogeshe akiwa mchanga ,amekua mtu mzima ndio maadili yanaonekana, amabae anasema sio maadili hao ndio wakiachwa na watoto wao wanawaza usheitwan

 3. Ndio inabidi tutambue na tukubali kwamba kila jambo lina wakati wake hasa kuhusu ukuwaji wa binaadam/ukiwa mtoto uliweza kutembea uchi bila shida na hakuna wa kukushangaa lakini jaribu leo ukiwa mtu mzima tukuone

 4. Iko fresh tu bongo usenge tu kla saa kiwaza ngono tu yaan mtoto acdeke.kwa baba ake ksa tu ana kubwambwa angekua wa kiume anadeka kwa mama ake hapo cjui mngeaema tena ukiona baba anawaka hisia za kmapenz kwa mwanae bac jua waz c yeye n Pepo

 5. Yani watu bwana…. « waheshimiwa ku tafsiri na kubadilisha mambo….» hamjambooooo
  Baba na mwanae kukua hivyo kuna shida gani???????
  Mkumbatie mwanoa na we binti mkumbatie babako…. huyo ndio rafiki yako wa kweliiiiiiiii….. ❤❤❤❤❤❤

 6. Mimi nilisha muona baba na mtoto wakivunja amri ya 6 hivyo tusikatae binti yako ukisha muona kwa macho ya kiutu uzima ameanza kuwa na hisia za kimwili Karibu kuepuka baadhi ya vitu na ukaribu usio wa lazima kama hivyo

 7. Halafu mbona huyo baba mwenyewe kama matingas hatuko ulaya hapa nifrika lazima mjijue asitake kuunga mkono mambo ya mbele kuiga ujinga tu hizo ndodalili mbaya kesho kapakatwa na baba wa mwenzie anaona sawa tu kwasababu alisha zoea et

 8. Sidhani hapa kama kuna ukakasi hata kidogo. Huyo ni baba ambaye yupo na binti yake aitwaye Caren sasa mtoto ameamua ‘kudeka’ kawa baba yake shida ipo wapi?! Wakati mwingine tuache kuhoji vitu vidogo vidogo namna hii wananzengo.

 9. Nakubaluana nawe Jackson magezi kwa sabb kwanza utambue wanaume maumbile yenu ni mafupi mno kwayo na mioyo ivo ivo. Utafanya alafu baada ya kitendo unaanza kujuta na kwenye kujuta unaendelea ndani kwa ndani alafu unajitia moyo kuwa hawanioni watu unaendeleza ka mchezo mpaka kanakomaa uwiiii mwaume hautakiwi kuwa karibu kiivyo na bindi yako ok

 10. Bin Maaruf Acha akili za kitoto, usi tafsri jambo kama lilivo ongeza akili ya ubongo wako, point hapo ilikua watu wanasema sio maadili,hivi mzazi unaweza mtamani mwanao? Kama mtoto wako ulie mzaa unaweza mtamani Basi hata mzazi wako hushindwi mtamani, kwahiyo wewe ukipiga picha na mama yako itakua ni maadili mabovu? Acheni akili fupi

 11. Watanzania sijui kwa nini tunapenda sana kuendekeza akili za kipuuzi maana Mimi binafsi sielewi hayo mashaka yanakuja vipi…..alafu pia hao ambao wanamashaka hawajiulizi aliepiga hio picha alikua hapo amekaa na wao??

 12. Huyu jamaa ni mlevi wa kupindukia ndio sababu ya kuachana kwakwe na jide imefikia hatua mbaka alikuwa anatembea na wananyakazi wa nyumbani lodge ya lad Jaydee kipindi kile pata picha mtu anaethubutu kutembea na wafanyakazi wake #mabaamedi #mento awezi shindwa kutembea hata na binti yake mlevi akishalewa awezi shindwa fanya chochote wakati wowote saa yeyote fikiria Kwa umri wa huyo binti siwakukaa na baba yake karibu hivyo hasa kipindi hiki cha baridi #atamwachaje_kwa_mfano

 13. Akili za kibongo zimekaa kizinzi sana ndiyo maana kila picha ya mwanaume na mwanamke tafsiri ya kwanza ni mahusiano ya kimapenzi,mara ngapi tumepiga picha tumewakumbatia wazazi wetu,au kwa sababu Gadner hana mke na binti yake ni binti wa pekee?kuishi kwa masharti na watoto kumesababisha waharibikiwe sana katika maisha.

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW