Habari

Picha ya Mh. Lissu akiwa hospitali baada ya kushambuliwa kwa risasi

Baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe jana kueleza kuwa wataanza kuonyesha picha za Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, hatimae leo picha hizo zimeonekana.

Mh. Lissu alipigwa risasi Septemba 7 mwaka huu na watu wasiojulikana eneo la ‘area D’ mjini Dodoma ambapo tangu kupata shambulio hilo picha ya mbunge huyo haijawahi kuonyeshwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika hivi: Madaktari wanatibu, ila Mungu anaponya.Tuendelee Tuendelee kumuombea @tundulissutz

Lissu yuko nchini Kenya kwaajili ya kupatiwa matibabu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents