Michezo

Picha: Yaliyojiri kwenye mechi ya Simba na Yanga zilizotoka sare ya mabao 3-3

Mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga Jumapili hii imemalizika kwa sare ya mabao 3-3 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Hiyo ilikuwa ni mechi iliyokuwa ushindani mkubwa ambapo Yanga katika kipindi kwa kwanza ilifanikiwa kuifunga Simba mabao matatu hali iliyowafanya mashabiki wa Simba wanyong’onyee kwa kuamini kuwa wamepoteza mechi hiyo.

Jerry Tegete akiwalaumu wachezaji wa ndani baada ya Simba kusawazisha goli 2 katika kipindi cha pili.
Mchezaji wa Yanga, Jerry Tegete akiwalaumu wachezaji wa ndani baada ya Simba kusawazisha goli la 2 katika kipindi cha pili

Mrisho Khalfan Ngassa ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwanyanyua mashabiki wa Jangwani kwa kufunga bao la kwanza katika dakika ya 15. Dakika ya 36, Hamisi Kiiza aliiandikia Yanga bao la pili katika mpira wa kurushwa na Mbuyu Twite.

Kipa wa Simba aliumia shingo baada ya kubabatizana na mchezaji wa Yanga katika harakati za kulinnda lango.
Kipa wa Simba aliumia shingo baada ya kubabatizana na mchezaji wa Yanga katika harakati za kulinda lango

Katika dalili ya wazi kuwa bahati ilikuwa kwa Hamisi Kiiza, mchezaji huyo aliitikisa tena nyavu ya Wekendu wa Msimbazi na kuifanya idadi ya magoli kuwa 3 bila, hali iliyoendelea hadi timu hizo zilipoenda mapumziko. Pamoja na Yanga kupata magoli matatu, walikitawala kipindi chote cha kwanza hali iliyowafanya Simba waonekane kama ‘Waanagenzi’ tu.

Mashabiki wa Simba wakiongozwa na Mwigizaji wa filamu nchini JB walikosa raha baada ya kufungwa bao 3 katika kipindi cha kwanza.
Mashabiki wa Simba wakiongozwa na muigizaji wa filamu nchini Jacob Stephen aka JB wakiwa na nyuso za huzuni na zilizokata tamaa baada baada ya Simba kufungwa mabao 3 katika kipindi cha kwanza

Kama vile waliamshwa usingizi, wachezaji wa Simba waliingia uwanjani kwenye kipindi cha pili wakiwa na nguvu za ajabu na kuanza mashambulizi yaliyoivunja ngome ya Yanga. Haikuchukua muda mrefu, nguvu mpya za Simba zikaanza kuzaa matunda.

Mashabiki wa Simba wakishangilia ushindi wa 3-3 baada ya mechi kumalizika.
Mashabiki wa Simba wakiwa wamepata nguvu mpya, wakishangilia

Katika dakika ya 54 tu, Betram Mombeki alifunga goli la kwanza la Simba. Wakati Yanga ikiwa inaanza kulionja joto la ghafla kutoka kwa Simba na kujipanga kulinda ngome yao isivunjwe tena, katika dakika ya 58 Joseph Owino aliandika bao la 2 lililozalishwa na krosi maridadi kutoka kwa Ramadhani Singano aka ‘Messi’.

Mashabiki wa Yanga awakuamini ka mpira umeisha kwa 3-3.
Mashabiki wa Yanga wakionekana kutoamini jinsi upepo ulivyobadilika

Goli la pili liliwapa nguvu zaidi Simba waliondelea kuwashambuliwa Yanga kwa kasi. Katika hatua hiyo wachezaji wa Yanga walianza kujichanganya na kuwadhoofisha zaidi hadi kumpa mwanya beki Kaze Gilbert kusawazisha goli la tatu na kuvifanya vibao vya magoli uwanjani humo kusomeka Yanga 3 – Simba 3.

Mashabiki wa Yanga na Simba wakitambiana baada ya Mechi kumalizika
Mashabiki wa Yanga na Simba wakitambiana baada ya mechi kumalizika

Tazama picha zaidi za mambo yalivyokuwa kwenye mechi hiyo.

Mrisho Khalfani Ngassa akijaribu kuitoka ngome ya Simba .
Mrisho Khalfani Ngassa akijaribu kuitoka ngome ya Simba

Mshabiki wa Yanga waliduwaa baada ya Simba kusawazisha mabao 3 katika kipindi cha pili.
Mashabiki wa Yanga waliduwaa baada ya Simba kusawazisha mabao 3 katika kipindi cha pili

Mwamuzi wa mchezo wa Simba na Yanga  Israel Nkongo akiingia  uwanjani kipindi cha pili.
Mwamuzi wa mchezo wa Simba na Yanga, Israel Nkongo akiingia uwanjani kipindi cha pili

Refa akitoa kadi ya njano kwa mchezaji wa Simba.
Refa akitoa kadi ya njano kwa mchezaji wa Simba

Shabiki ambae achoki kushangilia.
Shabiki ambaye achoki kushangilia

Shabiki namba moja wa Yanga akishindwa kuamini kama mchezo umeisha kwa goli 3-3.
Siamini: Shabiki namba moja wa Yanga akishindwa kuamini kama mchezo umeisha kwa goli 3-3

Wachezaji wa Yanga wakijadili baada ya kufungwa magoli katika kipindi cha pili.\
Kunani: Wachezaji wa Yanga wakijadili baada ya kufungwa goli la 2 katika kipindi cha pili

kumalizika-kwa-sare-ya-3-3..jpg”>Shabiki wa Yanga Athuman Kombo akilia baada ya mchezo wa Yanga na Simba kumalizika kwa sare ya 3-3.
Shabiki wa Yanga aitwaye Athuman Kombo akilia kwa uchungu baada ya mchezo wa Yanga na Simba kumalizika kwa sare ya 3-3

Watu walizimia kutoka na presha.
Ushabiki wa kweli: Watu walizimia kutokana na presha ya mchezo

Benzi la wachezaji wa Simba.
Benchi la wachezaji wa Simba

Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni akiongea na waandishi wa habari baada ya mechi kumalizika.
Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni akiongea na waandishi wa habari baada ya mechi kumalizika

Kocha Mkuu wa Yanga Ernie Brandts kulia na (2)
Kocha Mkuu wa Yanga Ernie Brandts akiwa na msemaji wa TFF

IMG_9240
Irene Uwoya, Mzee Yusuf na Shamsa Ford wakifuatilia mpira katika jukwaa la Yanga

IMG_9241

IMG_9242

IMG_9247

IMG_9248

IMG_9249

IMG_9250

IMG_9252

IMG_9253

IMG_9259

IMG_9261

IMG_9262

IMG_9263

IMG_9265

IMG_9267

IMG_9268

IMG_9269

IMG_9270

IMG_9272

IMG_9276

IMG_9279

IMG_9281

IMG_9285

IMG_9293

IMG_9306

IMG_9321

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents