Burudani

Picha: Yanayojiri kwenye ndege inayomzungusha Rihanna kwenye ziara ya 777, anazunguka na timu ya watu 240!!

Rihanna akiwa na marubani wa ndege ya tour yake

“Are you ready for Mexico? Are you ready for tequiiiiiiila? Sit down, buckle your seat belts, and let’s get drunk,” ni sauti ya Rihanna inayosikika kwenye ndege ya Boeing inayomzungusha kwenye ziara yake aliyoipa jina la 777. 777 maana yake ni siku 7 za tour katika majini 7 ya nchi 7 duniani.

Wakati ndege ikiwa angani mashabiki wa Rihanna waliopata bahati ya kualikwa kwenye tour hiyo pamoja na waandishi wa habari wapatao 150 kinachooendelea ni kula bata na mtungi kwa kwenda mbele.

Katika wakati mmoja safari hiyo iliingia dosari kidogo baada ya mwandishi mmoja kuamua kuvua nguo zake wakati ndege ikiwa hewani na kuamsha kelele na shangwe nyingi kwenye ndege hiyo.

Safari hiyo imeingiwa na dosari baada ya Rihanna kukataa kufanya interview na mwandishi yeyote na kumfanya mtangazaji huyo wa Fox FM ya mjini Melbourne, Australia kuvua nguo zake.

Wengine wanalalamika kuwa Rihanna amekuwa akitumia muda mwingi amejifungia kwenye chumba cha dharura.Pia huduma ya chakuka kwenye ndege hiyo imekuwa ikilalamikiwa na watu hao wanaodai kulishwa vyakula vya ajabu ajabu.

Wengine wanadai kuwa hawana muda wa kupumzika licha kufikia kwenye hoteli za kifahari ambako hulala kwa saa mbili au tatu tu kabla ya kuamshwa tena kuanza safari ya nchi nyingine.

Leo Rihanna atakuwa na show jijini London na tayari ameshaperfom Mexico City, Toronto, Stockhom, Berlin na Paris.

Hizi ni baadhi ya picha za ndani ya ndege hiyo na zile anazotumbuiza kwenye ziara hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents