Michezo

Picha: Yaya Toure akaribishwa kwa kishindo  Olympiacos, mamia ya washabiki wajitokeza

Mamia ya washabiki wa klabu ya Olympiacos wakiwa na mishumaa ya moto usiku wa jana wamejitokeza kumpokea aliyekuwa nyota wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure ambaye amerejea ndani ya timu hiyo baada ya kupita miaka 12 toka kuondoka kwake.

Kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 35 amepokewa na washabiki wa Olympiacos kwenye dimba la Karaskaikis hapo jana siku ya Jumapili huku akishuhudia timu hiyo ikiibuka na ushindi wa jumla ya mabao 5 – 0 dhidi ya vibonde wa ligi kuu ya Ugiriki klabu ya Giannena.

Ture amewahi kuichezea klabu hiyo msimu wa mwaka 2005/06 na amekuwa mchezaji huru tangu aachane na mabingwa wa ligi kuu England timu ya Manchester City.

Former Manchester City star Toure returns to Olympiacos after leaving them back in 2006

Olympiacos imemaliza msimu wa michuano ya Europa League baada ya kuifunga Burnley jumla ya mabao 4-2 kwa ‘aggregate’.

Kwa upande wake Toure amesema kuwa alipata ofa kutoka kwenye klabu mbalimbali kabla ya kufanya maamuzi ya kuichagua Olympiacos.

”Nilipata ofa ya kuchezea klabu mbalimbali kabla hata ya kuichagua Olympiacos. Si wezi kusubiri kuisaidia klabu kutwaa mataji yenye mashabiki wazuri kama hii, nadhani Olympiacos inastahili,” ameandika Toure kwenye tovuti yake.

A lot of fans turned out to see him and reports claim he will be paid £2.2 for the season

Ingawa hakuna maelezo ya kile atakacholipwa lakini tovuti ya ya michezo ya ‘Sport24’ kutoka nchini Ugiriki imesema kuwa Toure atalipwa pauni milioni 2.2 kwa msimu mmoja ukijumlisha pauni milioni 1.8 ya kusaini kama  ‘bonus’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents