AwardsBurudani

Picha za Kili Music Awards 2011 Launch

kiliawards_banner

Tuzo za kipekee za muziki Tanzania, Kilimanjaro Music Awards jana zilizinduliwa rasmi kwa mwaka wa 2011 katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam usiku wa tarehe 19 Januari.

 

Zoezi hilo liliwakutanisha wadau mbalimbali wa sanaa na muziki wakiwemo waigiza filamu Bongo, wasanii wa rap na waimbaji, wana habari pamoja na wadau mbalimbali wa muziki kutoka sehemu tofauti za Tanzania.

Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akizungumza katika uzinduzi huo, aliahidi kwamba mwaka huu tuzo zitaboresha zaidi. Akiongea na wageni waalikwa, alisema kuwa mwaka jana tuzo zilipata mafanikio makubwa ila mwaka huu Tanzania Breweries kupitia kinyaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager wamejipanga vizuri ili kuboresha zaidi mwaka huu.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro,George Kavishe aliongezea kwa kusema Tanzania Breweries kwa kupitia chapa yake ya Kilimanjaro watajitahidi kuendelea kuleta mabadiliko katika ulimwengu wa sanaa hususan wanamuziki kwa dhumuni la kukuza na kuboresha vipaji.

Kifuatacho sasa ni mkutano wa the Kili music awards Academy na baada ya hapo utambulizi rasmi wa wasanii kupitia nyimbo zao ambao watakuwa wakiwania tuzo hizo za Kili.

{gallery}2010/kililaunch{/gallery}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents