Habari

Picha:Mabanda ya wafanyabiashara wa soko la Karume yateketea kwa moto

Moto mkubwa umetetekeza kabisa soko kubwa kabisa la mitumba la karume jijini Dar es Salaam usiku wa Jumatano, na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara wote wa soko hilo.

Baadhi ya mabanda yakiteketea kwa moto
Baadhi ya mabanda yakiteketea kwa moto

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamedai moto huo ulianza kuteketeza mabanda hayo majira ya saa 4 usiku, huku wakijaribu kutafuta msaada kuuzima bila mafanikio yeyote.

Wazima moto walifanikiwa kuudhibiti moto uloweza kufikia karibu na kiwanda cha Breweries, lakini haujasababisha hasara yeyote katika nyumba za jirani wa soko hilo kwa mujibu wa mwandishi habari wa Raia Mwema Mbaraka Islam alipozungumza na Sauti ya Amerika.

Anasema hakuna kibada cha biashara kilichosalimika na hakuna mtu aliyefanikiwa kuokowa mali yake. Mfanya biashara Wilson magembe anasema amepoteza kila kitu na ilikuwa vigumu kuweza kuchukua bidhaa zao kwa sababu moto uliwaka kwa haraka sana.

Moto mkubwa
Moto mkubwa
k

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents