Burudani

Picha/Video: Chin Beez alivyowasha moto Tandika katika ‘Road Experience’

Chin Beez ametengeneza historia ya kuwa msanii wa kwanza Bongo kufanya ziara ya show kwa mashabiki wake mitaani bure ambapo ameipa jina la Road Experience.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anahit na ngoma yake mpya, Nyonga Nyonga ameanza ziara hiyo Ijumaa hii katika eneo la Tandika Sokoni mjini Dar es Salaam ambapo pia amefanikiwa kutoa zawadi mbalimbali kwa mashabiki wake hao ambao walihudhuria show hiyo.

Hata hivyo Chin ambaye yupo chini ya kampuni ya Wanene Entertainment alipoongea na Bongo5 kabla ya show hiyo amesema kuwa anatarajia kuzunguka mikoa mingi ya Tanzania kadri itakavyowezekana ilimradi awafikie mashabiki wake na atakuwa akifanya show hizo bila kiingilio.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents