Bongo5 Exclusives

Picha/Video: Ephraim Kibonde akamatwa na polisi kwa kusababisha ajali na kukaidi amri ya trafiki

Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Ephrain Kibonde leo ameshuhudia jinsi ambavyo mkono wa sheria ulivyo mrefu hata kwa mtu maarufu kama yeye alipojikuta kwenye wakati mgumu baada ya kusababisha ajali na kushindwa kutoa ushirikiano kwa polisi wa barabarani.

Picha ya mtangazaji huyo akiwa amepigwa ‘Tanganyika Jeki’ na polisi wa barabarani imeenea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii pamoja na maelezo ya mtu aliyeshuhudia tukio hilo.

Kibonde
Kibonde akiwa amepigwa Tanganyika Jeki

Taarifa hiyo inasema:

Kibonde wa Clouds anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho. Amemgonga dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walipofika kupima ajali, Kibonde karudi nyuma kaendesha gari lake kasepa! Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia. Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge.

Trafiki aliingia katika gari lake nakumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde kagoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake, trafiki naye kagoma kushuka. Mchezo ulioendelea Kibonde aliondoa gari na kuanza kupiga misele, akizunguka mitaa akiwa na trafiki huyo! Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kila kiunga cha jiji hususani eneo la Mwenge na Ubungo.

Hayawi, hayawi yakawa, Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo nikashuhudia senema ya Kibonde na trafiki! Trafiki wa kike aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde iliyokuwa kasi, gari hiyo haikuonesha dalili za kupunguza mwendo. Trafiki alikomaa kusimama mkono wake ukiwa juu kuashiria kumtaka Kibonde asimame huku akipaza sauti ktk radio call akisema ananigonga, afande, ananigonga!

Akiwa ktk hali hiyo, kuna gari ilikotokea sikujua ikakatisha kati ya trafiki na gari ya Kibonde ndiyo ikawa kigingi cha gari ya Kibonde na kutiwa mbaroni! Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki ambapo kwa sasa amepelekwa Oystabay! Kwa utafiti wangu kidogo nilioufanya nikifukuzana na muda kuwahi kanisani, ni kwamba Kibonde na watu wengine aliokuwanao ndani ya gari lake walikuwa ‘TINGASI’!

Maelezo ya mtu mwingine aliyeshuhudia tukio hilo yanasema: Kagonga gari ya mzungu mmoja ilikuwa mbele yake, Mzungu kashuka garini traffick wakaja na kibonde kashuka eti anaanza kumletea kibesi mzungu kwakuona sijui yule mgeni nchi hii akaanza kumsukuma mzungu mwenyewe mrefu kibonde anaonekana kama mbilikimo kwake trafick wanamzuia akaanza kuwafanyia fujo uuuuh yn kasombwa Tanganyika jeki kapelekwa kituoni.

Jitihada za kumtafuta Kibonde kwa simu zimeshindikana kwakuwa simu yake haipatikani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents