HabariPromotion

Picha/Video: Famous Furniture watua Dar, wakali wa magodoro ya Sealy na masofa ya La-Z-Boy

Kampuni ya Famous Furniture imefungua duka lake Mlimani City, Dar es salaam, Tanzania kwa ajili ya wanaopenda kuishi maisha yasiyo na karaha na kwa starehe.

Mmoja kati ya mameneja wa kampuni hiyo wakitoa maelezo mapema leo kwa wateja wao ambao walihudhuria uzinduzi wa duka hilo

Famous Furniture watakuwa ni wasambazaji rasmi magodoro na vitanda vya Sealy Posturepedic pamoja na sofa na viti vya La-Z-Boy nchini.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jioni ya leo katika ufunguzi wa duka hilo,  ,alisema Sealy ina vitanda na magodoro ya aina mbalimbali yanayokidhi mahitaji ya kiafya na starehe na yanayodumu kwa muda mrefu.

“Sealy ina uzoefu wa utengenezaji wa magodoro na vitanda kwa zaidi ya miaka 100, na kwa sasa ndiyo chapa inayoongoza kwa kutengeneza vitanda na magodoro bora kabisa duniani kote. Vitanda vya Sealy vimetengenezwa na wabobeaji wa afya ya mfupa ili kukupatia starehe, mfumo bora wa egemezi yote haya yakiwa kuhakikisha unapata usingizi mzuri na wenye afya,” alisema Dhaesee.

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kwanza kushoto) akitaniana jambo na rafiki yake aliyelala katika kiti maalum ambacho pia kinapatikana ndani ya duka hilo.

Aliongeza “Zaidi ya watu miloni 40 duniani wanapata usingizi mzuri na kuamka wenye afya kwa sababu ya kutumia bidhaa za Seay Tunahakksha usiku wako unakuwa wenye pumziko na amani. Usingizi mzuri hupoza mwili, unakupa nguvu, unahakikisha unakua vyema na afya nzuri huku akili yako ikizidi kujenga vizuri. Kumbuka, unatumia theluthi ya maisha yako yote kwenye usingizi. Leo hii, kuna bidhaa mbalimbali za Sealy unazoweza kuchagua lakini lengo letu ni moja; kuhakikisha tunakuwa sababu ya wewe kuwa na maisha yenye starehe,”

Alisema Fenicha za La—Z—Boy zinatengenezwa na kusambazwa kwa leseni katika nchi nyingi duniani.

“La—Z— Boy ina haki miliki za US na kimataifa kwenye miundo zaidi ya 200. Dizaini ya kwanza ilitengenezwa mwaka 1928 na tangia hapo, wamekuwa ni mabalozi ”maisha ya starehe” wanaoongoza duniani,” alisema Dhaesee.

Naye  Ryan Beattie kutoka Bravo Group, msambazaji wa La—Z—Boy kutoka Famous Furniture alisema binadamu hutumia muda mwingi wakiwa wamekaa chini, hii ndio ya sababu ya wabunifu, watafiti na wataalamu wa afya kuumiza vichwa kutoa bidhaa zitakazoleta starehe katika mikao.

“Unahitaji kukaa kwenye viti bora na vizuri vinavyokujenga kiafya.  Starehe ya mkao sio katika muonekano tu hata aina ya kitu unachokalia kinakupa starehe ya mwili na mfumo bora wa egemezi, hasa kama unakaa kwa muda mrefu,” alisema Beattie.

Kuhusu Famous Furniture Ltd

Famous Furniture Limited (iliyosajiliwa na namba 135127) iliona umuhimu wa kutambulisha bidhaa bora za nyumbani ili kukidhi soko linalokuwa la Tanzania. Bidhaa bora za La-Z-Boy zitaboresha mwonekano wa nyumba yako na starehe yako ya mkao wakati magodoro ya Sealy posturepedic yatahakikisha usingizi wenye afya. Na sasa vyote hivi vinapatikana katika duka namba 47, Mlimani City. Wataalamu wetu wapo tayari kusikia mahitaji yako na kuyafanyia kazi. Famous Furniture inatarajia kufungua maduka mengine matano (5) nchini kote kabla ya mwisho wa mwaka 2018.

Famous Furniture ni kampuni iliyo chini ya Bravo Group Manufacturing (Pty) Ltd yenye viwanda 7 Afrika Kusini na inayoongeza kwa kuwa na bidhaa bora za chumbani na sebuleni.









 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents