Habari

Picha/Video: Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi azindua mradi wa tatu wa maendeleo Zanzibar

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Zanzibar, Ayob Mahamud, amezindua rasmi mradi mpya  wa maendeleo kwa Jamii kwa ajili ya kujenga na kuziendeleza shule zilizopo katika mkoa wake.

Mradi huo unaendeshwa kupitia kapeni yake iliyozinduliwa hivi karibuni iitwayo ‘Mimi na Wewe’. Kupitia mradi huo RC Ayoubu ameanza ujenzi huo kwa kujenga vyumba vya madarasa katika shule madarasa ya msingi Kijito Upele ambayo yalikuwa wameacha kuendelezwa kwa zaidi ya miaka mitandao.


RC Ayoub akiongea na wananchi wake katika shule ya msingi Kijiko Upele

Katika uzinduzi huu Mamlaka ya Bima Tanzania kanda ya Zanzibar (TIRA) kupitia kwa Mwenyekiti wake, Juma amechangia jumla ya mabati 62 ilikuwezekwa katika vyumba hivyo vya madarasa.

Akizindua ujenzi huo RC Ayoubu amewataka wanannhi wake kuhakikisha wanashiriki katika kuleta maendeleo na kutumia umoja ambao ulianzishwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Amani Abed Karume.

Na Laila Sued na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents