Soka saa 24!

PIGO JUU YA PIGO: Wezi waiba vitu vya thamani na pesa taslimu kwenye jumba la kifahari la mzee Mengi

Ikiwa zimepita siku mbili baada ya mfanyabiashara maarufu Tanzania, marehemu Reginald Abraham Mengi kuzikwa, wezi wameiba vitu vya thamani na fedha taslimu kijijini kwake Nkuu, Machame, Kilimanjaro kwenye nyumba yake ya kifahari.

Vitu hivyo vinavyodaiwa kuibiwa ni mikufu ya dhahabu, kompyuta pamoja na fedha taslimu ambazo kiwango chake bado hakijaelezwa.

Akithibitisha taarifa hizo, Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah amesema kuwa mpaka sasa Polisi wanawashikilia watu wawili wanaoshukiwa kuhusika na wizi huo.

Ni kweli nyumbani kwa Mengi kumeibiwa,” amesema Kamanda Issah na kueleza kuwa tukio hilo huenda limefanywa na watu wanaodaiwa kuwa wa ndani na familia hiyo na kwamba taarifa za awali za uchunguzi zinaonyesha walitokea jijini Dar es Salaam.

Vitu hivyo vinasemekana kuwa ni mali ya Wanafamilia na waombolezaji na zilikuwa katika jumba la kifahari la mzee Mengi, wakati wa mazishi ya bilionea huyo yaliyofanyika Alhamisi iliyopita.

Chanzo: The Citizen .

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW