Technology

Pigo lingine kwa watumiaji wa simu za Huawei latangazwa, Facebook, WhatsApp na Instagram wajiweka kando

Kampuni ya Facebook imetangaza rasmi kuzuia huduma wezeshi (Apps) zao kufanya kazi kwenye simu za Huawei.

Zuio hilo linakuja katika vita baridi vya kiuchumi vinavyoendelea baina ya Marekani na China.

Hatua hiyo ya zuio inakuja baada ya Mwezi Mei serikali ya Marekani kuzuia kampuni za Marekani ikiwemo Google kutumia huduma za Huawei kutoka China, ikieleza ni sababu za kiusalama.

Zuio hilo linalenga huduma mama ya Facebook na nyingine kutoka kwa kampuni washirika ambazo ni WhatsApp na Instagram.

Kwasasa watu ambao tayari wamenunua simu za Huawei na wanapata huduma husika wataendelea kuzitumia isipokuwa wale watakaonunua matoleo mapya.

Facebook imesema pia itaendelea kusambaza huduma za kuweka mambo mapya (updates) kwa wamiliki wa sasa wa simu za Huawei.

Kwa upande mwingine, Kampuni ya Huawei haijatoa taarifa yoyote kuhusu uamuzi huo uliotolewa na Facebook.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents