PiliPili kuachia mbili kwa mpigo

PiliPili kuachia mbili kwa mpigo
Kampuni ya PiliPili Entertainment ambayo
imewadhamini wasanii Baby Madaha na Feisal Ismail, imetangaza kufanya
uzinduzi wa albamu mbili za wasanii hao Mei 30

Akizungumza jana
katika mkutano na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye
Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
hiyo, Nilesh Bhatt, amesema uzinduzi huo utafanyika katika Hoteli ya
Kilimanjaro Kempinski, jijini Dar es Salaam.

Amezitaja albamu hizo kuwa ni Amour ya Madaha na Hope ya Feisal, zote
zikiwa zimerekodiwa katika hadhi ya kimataifa, chini ya uongozi wa Pili
–Pili Entertainment, nchini India.

“Albamu hizo mpya zilizorekodiwa katika video na redio tayari zimeanza
kushika katika soko la muziki hivyo ni kazi ya kujivunia,” alisema
Bhatt.

Machi 16 mwaka huu wasanii hao ambao ni zao la Bongo Star Seach (BSS),
walikwenda nchini India kufanya kazi ya kurekodi video na nyimbo zao
kwa muda wa wiki mbili.

Uzinduzi huo unatarajiwa kuzinduliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara,
Dk. Mary Nagu. Na wadhamini wa uzinduzi huo ni Shoprite, Lesso na Jil-
Jil.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents