Habari

Pinda Acharukia Semina Mashangingi

Hatimaye, Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha walipa kodi juu ya matumizi makubwa yasiyo ya lazima serikalini katika ununuzi wa magari ya kifahari maarufu kwa jina la mashangingi na sasa ununuzi wake utapunguzwa kwa kiwango kikubwa.

Hatimaye, Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha walipa kodi juu ya matumizi makubwa yasiyo ya lazima serikalini katika ununuzi wa magari ya kifahari maarufu kwa jina la mashangingi na sasa ununuzi wake utapunguzwa kwa kiwango kikubwa.

Uamuzi wa kupunguza ununuzi ya magari hayo ulitolewa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati wa mkutano wake na makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu wote nchini uliofanyika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka kila mmoja mwaka baada ya mwaka kupunguza idadi ya ununuzi wa magari hayo.

Badala yake, Pinda alisema fedha zitakazookolewa kwenye manunuzi hayo zielekezwe katika ununuzi wa pembejeo za kilimo kwa lengo la kupunguza umaskini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kutathmini hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini nchini (Mkukuta) na kubuni namna ya kuongeza kasi ya kuondoa vikwazo vilivyopo katika kupunguza umaskini wa kipato wa mtu binasfi.

Alisema serikali imeamua kupunguza ununuzi wa magari ya kifahari kwa kwa kila mwaka ili fedha hizo zielekezwe kununulia pembejeo za kilimo ili kuangalia kwa namna gani nchi itafikia malengo ya Mkukuta iliyojiwekea ifikapo mwaka 2010.

Alisema hatua za kupunguza ununuzi wa magari ya kifahari zitasaidia kupata fedha zaidi za kuelekezwa katika sekta ya kilimo ambayo ina asilimia 80 ya rasilimali watu, na kwamba baadaye tathmini ya ukuaji wa kipato cha mtu mmoja mmoja itafanyika ili kujua mafanikio yaliyofikiwa.

Alisema umaskini unapaswa kupungua kutoka asilimia 38.6 kwa watu wa maeneo ya vijijini na kufikia asilimia 24 ifikapo mwaka 2010.

Serikali imekuwa ikilalamikiwa kwa kutumia fedha nyingi kununulia magari hayo kwa ajili ya maofisa wake waandamizi, ambayo licha ya kugharimu fedha nyingi, pia yanasababisha matumizi makubwa yasiyo ya lazima hasa mafuta na gharama za matengenezo.

Alisema hata yeye binafsi haoni sababu ya kutembelea gari la kifahari wakati kuna wananchi wanaoishi kwa kutegemea mlo mmoja kwa siku huku wakiendelea kusota kutokana na uduni wa maisha hasa katika maeneo ya vijijini.

Sambamba na hilo, Waziri Mkuu aliwataka viongozi hao ambao ni dira ya uwajibikaji katika wizara zao kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao na kupiga vita rushwa katika wizara wanazosimamia ili kuondoa vipingamizi vya maendeleo vinavyosababisha woga wa uwekezaji katika sekta za uzalishaji.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents