Siasa

Pinda ‘amfuta’ kazi mtendaji

MTENDAJI wa Kata ya Kabwe wilayani hapa, amejikuta katika wakati mgumu baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumsimamisha kazi kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Angela Semaya, Nkasi

 

 

 
MTENDAJI wa Kata ya Kabwe wilayani hapa, amejikuta katika wakati mgumu baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumsimamisha kazi kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake.

 

Waziri Mkuu aliwataka watendaji kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa kuzibandika katika sehemu mbalimbali, ikiwamo misikitini, makanisani, pamoja na kuwataka wananchi kugoma kama watendaji hao hawataki kutoa taarifa hizo.

 

Charles Sichela alijikuta akipoteza kazi baada ya wananchi kumtuhumu kushindwa kutoa taarifa za mapato na matumizi ya michango wa shule za sekondari. Pinda aliamua kumuita Sichela na kumhoji kama tuhuma hizo ni kweli na alikiri kweli hajatoa taarifa ya mapato na matumizi kwa mwaka jana.

 

Diwani wa kata hiyo, Asante Lubisha (Chadema) alipoulizwa, alisema katika taarifa ya mwaka 2004 inaonyesha zilikuwa Sh milioni 34, lakini tangu mtendaji huyo aingie anashangaa taarifa ya matumizi na mapato kuna Sh milioni tano, hali ambayo inakatisha tamaa.

 

Sichela, ambaye aliingia madarakani mwaka juzi, alimweleza Waziri Mkuu kuwa hajatoa taarifa kwa sababu wanasubiri taarifa ya ukaguzi ndipo wapite kijiji hadi kijiji kuwaeleza wananchi. Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema mtendaji huyo hajui kazi kwani kwa kawaida mtendaji hawezi kukaa mwaka mzima bila kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa wananchi.

 

“Haya kweli ni ya kujitakia mwenyewe, kuanzia sasa mtendaji huyu amesimamishwa kazi,” alisema. Waziri Mkuu alimueleza Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Christina Midelo, kufanya kazi ya kuchunguza na hatua zaidi zitachukuliwa na kwamba hata kama mtendaji huyo amekula fedha, atarudisha kila senti. “Ole wake kama amekula, fedha zitarudi kila senti.

 

Haiwezekani, kuanzia sasa taarifa za mapato na matumizi ya michango zibandikwe sehemu mbalimbali sokoni, kanisani, msikitini,” alisema. “Si haki kama wananchi hawapewi taarifa zozote za michango yao.”

 

“Wananchi gomeni kama watendaji hawataki kutoa taarifa na serikali itawashughulika nao…kwa mtendaji huyu wa kata hapana, yeye ndio anatakiwa kuwa kinara wa shughuli hizi,” alisema. Alitaka pia Mkuu wa Mkoa kuunda timu itakayopita kwa wananchi kuangalia kama wanapewa taarifa ya mapato na matumizi.

 

 

 

Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents