Pinda Asema Semina No Wizarani

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amepiga marufuku wizara kuendesha warsha, semina na makongamano na kwamba kila anayetaka kufanya hivyo sasa atalazimika kupata kibali chake.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amepiga marufuku wizara kuendesha warsha, semina na makongamano na kwamba kila anayetaka kufanya hivyo sasa atalazimika kupata kibali chake.

Waziri Mkuu alitoa amri hiyo juzi wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mtejeta, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma kwa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Niliwaambia watu wa wizara, wakitaka kuandaa mambo hayo, walete kwanza michanganuo kwangu… wizara moja ilinitetea, kutazama nikakuta kuwa itatumia Shilingi bilioni nne kuendeshea warsha,“ alisema kwa mshangao.

Aliongeza kuwa, kiasi hicho alifikiria ni matrekta mangapi yangenunuliwa na kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kuinua kilimo.

Pinda alisema warsha kama hizo zikifanyika katika wizara 10, maana yake zitatumia Sh. bilioni 40 na kwamba hiyo ni njia ya kutaka posho.

“Na walivyo wajanja, wamekuwa wakinialika kufungua na mimi nimekuwa mnjanja, sikubali. Tutawanyima pesa hizo zitumike katika shughuli za maendeleo,“ alisisitiza.

Alisema kuanzia sasa, michanganuo ya wizara zote, italazimika kupitia kwake na kwamba ataisoma na kuruhusu kufanyika kwa semina, warsha, makongamano ambayo yataleta tija.

Alisema kuna baadhi ya wizara huandaa hadi semina za ndani ya idara na pia akapiga marufuku suala la kupeana motisha ambao ni utaratibu unaolenga kuwapatia watumishi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents