Pinda kupekecha Diamond Jubilee

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya kwanza ya bendi ya Akudo Impact ‘Wazee wa masauti’ utakaofanyika Mei 16, Ukumbi wa Diamond Jubilee

na Vumilia Kondo




WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya kwanza ya bendi ya Akudo Impact ‘Wazee wa masauti’ utakaofanyika Mei 16, Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijijni Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa tamasha hilo, Bahati Singh, alisema kuwa maandalizi yanakwenda vema ambapo siku hiyo kutakuwa na matukio muhimu manne yatakayosindikiza tamasha hilo, na Pinda amethibitisha kuhudhuria.

Singh aliyataja matukio hayo kuwa ni kusherehekea uzazi wa Akudo Impact kwa uongozi mpya ulioingia madarakani Mei 16 mwaka jana na ndoa rasmi kati ya Akudo na kundi la muziki wa taarab linalotesa hapa nchini kwa sasa, Jahazi Morden Taarab.

Matukio mengine ni mwanamuziki mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), Bozi Boziana, kukabidhi mikoba muhimu kwa Akudo Impact, ambayo pia hujulikana kama ‘Wana Pekecha pekecha’, ambayo itasaidia kuendeleza muziki wa dansi nchini na burudani ya aina yake kutoka Akudo.

Aidha, Singh aliongeza kuwa, kamati ya maandalizi imeahidi kutoa sh milioni moja kutoka kwenye mapato ya tamasha hilo, ili kununua vitanda na magodoro kwa ajili ya wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mwananyamala, kwa kuzingatia kuzaliwa pia kwa Akudo Impact kwa uongozi mpya.

Uzinduzi huo unatarajiwa kupambwa na Jahazi Modern Taarab ‘Wana nakshi nakshi’ na Bozi Boziana na kundi lake, ambaye anatarajiwa kutua nchini Mei 13 akiwa na wanamuziki wasiopungua saba.


 


Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents