Habari

Pingamizi la ruzuku la CUF ya Maalim Seif dhidi ya Prof Lipumba latupiliwa mbali

Ombi la pingamizi la Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad la kutaka Prof Lipumba asipate ruzuku za Chama hicho limetupiliwa mbali na Mahakama Kuu nchini Tanzania.

Prof Ibrahim Lipumba na Maalim Seif

Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi hilo leo tarehe 11 Agosti 2017, kufuatia Chama Cha CUF huko nyuma kufungua kesi ya msingi ya madai kuhusu wizi wa ruzuku na shauri dogo la kuweka zuio kutolewa kwa ruzuku ya chama kutokana na wizi wa shilingi milioni 369 ambazo zilidaiwa kuibwa na Prof Lipumba na kundi lake kwa kushirikiana na Msajili wa Vyama Vya Siasa.

Pingamizi hilo limedumu kwa miezi minne tangia Machi mwaka huu mpaka Agosti ambapo leo Mahakama Kuu imetupilia mbali zuio hilo lililowekwa na CUF upande wa Katibu Mkuu, hali ambayo inapelekea Msajili wa vyama vya siasa kuendelea kutoa ruzuku ya Chama hicho kwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa. Ibrahmi Lipumba na wananchama wake ambao wanamuunga mkono.

Tangu mwezi wa Septemba 24, 2016 baada ya Profesa Lipumba kudaiwa kufanya uvamizi wa ofisi za chama cha CUF Makao makuu Buguruni, Jijini Dar es salaam kinyume na sheria na taratibu baada ya Kujiuzulu kwa hiari yake na kuiacha ofisi hiyo takribani kwa kipindi cha mwaka mzima ndipo ulipoanza mgogoro kati ya pande mbili, upande unaomuunga mkono Prof Lipumba na upande unaomuunga mkono Maarim Seif jambo ambalo limesababisha madhara mengi ya moja kwa moja ndani ya chama hicho.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents