Burudani

Pink akingiwa kifua, ‘Hajacopy video ya Lulu Diva’ – Producer Mbezi

By  | 

Prodyuza Mbezi amefunguka na kusema msanii wake, Pink, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo ‘Unafeel Aje’, hakuiba idea kutoka kwenye video ya Lulu Diva ‘Usimuache’.

Pink

Akipiga stori na kipindi cha Compass Vibe, Mbezi amesema kwanza msanii hapaswi kumuingilia director ila anaweza akampa idea lakini na yeye akawa na kitu chake kingine anachokifikiria.

“Mimi sijaona tatizo sana kwa sababu video ya Lulu Diva nimemuona anatembea barabarani, video ya Pink amekaa kwenye bench barabarani, hivyo ni vitu viwili tofauti, yaani different idea, kwa hiyo sio tatizo.

“Director anaweza kukuambia wimbo wako unafaa katika script hii hapa, unajua video ni kama muziki codes zipo chache kwa hiyo unaweza ukakuta nyimbo nyingi zinatumia same code lakini mapingo yakawa tofauti au uimbaji unakuwa tofauti lakini hazijaongezwa ziko zile zile,” amesema na kuongeza.

“Same way kwenye director, unaweza kushoot angani lakini kama ni kwenye dunia yetu utakutana na changamoto zile zile, magari, nyumba, barabara. Kwa hiyo kama utatumia gari je wimbo wako unakuruhusu kufanya hivyo,” ameeleza Mbezi.

Kwa upande wake Pink amesema kwa sasa ameamua kuanza kuuza nyimbo zake katika mtandao kitu ambacho hapo awali halikuwa hafanyi ili kujitangaza zaidi.

“Mwanzoni tulikuwa hatuuzi kwa sababu mimi bado ni msanii mchanga mashabiki wanataka kunisikia na wapate nyimbo zangu bure, lakini sasa hivi meneja wangu amewaamini Wasafi,” amesema Pink.

Kuhusu ukaribu wake na prodyuza Mbezi, Pink amesema yeye amemuamini sana prodyuza huyo na anapenda kufanya nae kazi.

By Peter Akaro

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments