Michezo

Pochettino afunguka kwa mara ya kwanza kuhusu kurithi mikoba ya Zidane ndani ya Madrid

Kocha wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino, amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuenea kwa tetesi za kuwa kwenye mipango ya Rais wa Real Madrid Florentino Perez kufundisha timu hiyo.

Pochettino amekuwa akitajwa kutakiwa kurithi mikoba ya Zinedine Zidane aliyetangaza kujiuzulu kuifundisha Madrid Alhamisi hii. Akiongea na El Confidencial, Pochettino anafuraha kubwa kuifundisha Tottenham kwa kuwa bado wanafuraha na yeye kuendelea kuifundisha timu hiyo na pia anamkataba nao mrefu.

“Nimekuwa mvumilivu kwa muda wote katika hatua yangu ni sehemu ya kazi ya kusisimua, ninafurahi kuwa watu wa Tottenham wanafuraha na mimi, Kitu muhimu zaidi ni kufurahia muda huu,” amesema kocha huyo.

“Sio juu yangu. Dhamira yangu ni ya juu. Tuache mambo yaende. Tunafurahia wakati huo na nini kitatokea. Nina furaha sana kuwa Tottenham kwa sababu waniruhusu mimi kufanya kazi na tunakua pamoja. Sasa nataka kuzingatia kupanga mipango ya msimu ujao, na kuweka mbali kila kitu kinachozungumzwa,” ameongeza.

Mei 24, 2018 Pochettino aliongeza mkataba wa miaka mitano kuendelea kuifundisha Spurs ambao utafikia ukingoni mwaka 2023.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents