Michezo

Pochettino awatolea uvivu vijana wake ‘Kama unashindwa mechi kama hii ya PSV hustahili kuwepo Champions League’

Meneja wa klabu ya Tottenham, Mauricio Pochettino amewaambia wachezaji wake kuwa kama wameshindwa kupata ushindi mbele ya timu dhaifu kama PSV Eindhoven ambayo inaburuza mkia kwenye msimamo wa ‘group B’ basi hawastahili kuendelea kuwepo kwenye michuano hiyo ya UEFA Champions League.

Pochettino does not believe Tottenham will make it out of their Champions League group now

Pochettino ameamua kuwaambia maneno hayo baada ya kushuhudia dakika ya 87, PSV wakisawazisha na mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2 – 2 baada ya kuongo za kwa muda wato kupitia mabao ya Lucas Moura na Harry Kane huku mchezaji wake Hugo Lloris akitolewa nje kwa kadi nyekundu.

”Mapema tu, tunaonekana tunaondolewa, tuna pointi moja kwenye michezo mitatu. Hakika tupo kwenye wakati mgumu tunahitaji kushinda michezo mitatu,” amesema Pochettino.

Pochettino ameongeza ”Kama unashindwa kushinda mchezo kama huu basi hustahili kuendelea kuwepo kwenye michuano hii ya Champions League. Kama unacheza vizuri na unautawala mchezo na kufanikiwa kutengeneza nafasi nyingi kisha unashindwa kushinda, mechi ilikuwa wazi kabisa.”

Meneja huyo ameshindwa kumlaumu nahodha wake, Lloris kwa kupata kadi nyekundu ya moja kwa moja na kusababisha kwa kiasi kikubwa mechi hiyo kumalizika kwa matokeo hayo na hivyo kukosekana kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya PSV kwenye dimba la Wembley mwezi ujao.

”Simtupii lawama mchezaji yoyote, mimi ndiyo ninayestahili kuwajibika kwa kushindwa kushinda na kama unahitaji kumtupia mtu lawama nilaumu mimi.”

”Hugo hastahili kuomba radhi haikuwa bahati mbaya bali ilikuwa kwenye harakati ambapo chochote kingeweza kutokea kwenye mchezo wa soka.”

”Tunakitu cha kuonyesha kuwa sisi na Barcelona ni sawa, tutakutana tena na PSV na kunauwezekano mkubwa wa kushinda.”

The Tottenham players fell to the pitch in disappointment after Wednesday's draw in Holland

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents