Pochi Yawatoa Roho Maskini

Vijana wawili wanaotuhumiwa kuwa ni wameshambuliwa na wananchi hadi kufa baada ya kumpora abiria mkoba wake akiwa ndani ya daladala tukio lilitokea maeneo ya Manzese Argentina

Vijana wawili wanaotuhumiwa kuwa ni wameshambuliwa na wananchi hadi kufa baada ya kumpora abiria mkoba wake akiwa ndani ya daladala tukio lilitokea maeneo ya Manzese Argentina.



Vijana hao waliokufa papo hapo mmoja ametambulika kwa jina la Ramadhan Abbas (28) na mwingine mwanaume ambaye hajatambuliwa jina lake anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 30 wenye sifa ya kuvizia maeneo hayo na kuhatarisha maisha yao kwa kukwapua mali za raia.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum Dar es Salaam, Jamal Rwambow amesema kuwa tukio hilo limetokea jana nyakati za saa 4 usiku maeneo hayo na maiti zao wamehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Mwananyamala na polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.



Katika tukio linguine lililojiri maeneo ya Ubungo, wakazi wanne wa jijini wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa wakimiliki kiwanda cha kutengeneza ‘konyagi mwitu’ yaani Bangi.



Aidha Kamanda Rwambow amesema kuwa watuhumiwa hao walinaswa jana saa 5 asubuhi, Ubungo Kibangu na Kimara mwisho.



Amesema watuhumiwa hao walinaswa na polisi wa doria wakiwa na bangi kete 14, gongo lita 4, chupa tisa tupu za konyagi na boksi moja la konyagi lenye chupa 11. Aliyataja majina ya watuhumiwa ni pamoja na Desdelu Shirima (35), Ally Rajabu (24), Said Juma (32) na Rashid Abdalah (23).Watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents