Michezo

Pogba aelezea anavyojisikia katika safari ya Manchester kuifuata Juventus “Turin ni kama nyumbani”

Pogba aelezea safari ya Manchester kuifuata Juventus "Turin ni kama nyumbani"

Kiungo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa amefunguka jinsi anavyojisikia katika safari yao ya kuifuata klabu ya Juventus mjini Turin katika mchezo wao wa marudiano kwenye michuano ya UEFA Champion League.

Pogba aliongea hayo wakati akiongea na kituo cha RMC baada ya kuulizwa anajisikiaje safari yake ya kuifuata Juventus ikiwa ndio mara ya kwanza tangu ajiunge na United akitokea kwa wababe hao wa Turin.

Ikumbukwe kuwa Pogba alijiunga na United akitokea Juve kwa uhamisho uliovunja rekodi akinunuliwa kwa kiasi cha Euro milioni 89 na kufanikiwa kuisaidia Manchester kutwaa mataji kadhaa ikiwemo UEFA europa league pamoja na mataji mengine mawili kutoka nchini Uingereza.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika dimba la Old Trafford nyumbani kwa Manchester ambapo Juventus walifanikiwa kushinda mchezo huo kwa goli moja lililofungwa na Dyabala.

Na katika kundi hilo ambalo ni H Juventus wanaongoza kwa kuwa na alama 9 kwa kufanikiwa kushinda michezo yote mitatu huku nafasi ya pili ikiwa ni United wakiwa na alama 4 wakishinda mchezo mmoja wakipoteza mmoja na kupata sare mmoja,kama inavyoonekana hapa:-

Pogba alisema ” Nilitarajia hiki, ilikuwa ni wazi kabisa,” alisema Pogba “Nilisema kuhusu hilo na nilimwambia ndugu yangu mwisho wa majira ya joto Nilimwambia hivi ‘Fikiria tukawa katika kundi moja kama Juve.’

“Kwangu mimi, ni furaha Turin ni nyumba kwangu ndio sehemu pekee ambayo nilifunga goli langu la kwanza la kimataifa.”

Pogba aliongeza kuwa aliendelea kuwasiliana na baadhi ya wachezaji wenzake wa zamani wa Juventus na amejifunza kutoka kwa wachezaji hao wakongwe ikiwa ni pamoja na Andrea Pirlo. wengine ni “Juan Cuadrado, Paolo Dybala, Leonardo Bonucci  Nasikia kutoka kwao, tunazungumza mara kwa mara Tulikuwa familia, na kwa kweli tunaendelea kuwasiliana,” alisema.

“Unapokuwa pamoja na wachezaji kama Pirlo, Gigi Buffon au Giorgio Chiellini, unaweza kujifunza tu, Kila siku, katika mazoezi, unajaribu kuwaangalia, Hata kama mchezaji aliye imara, unaweza kujifunza kutoka kwa watu hao.”

Pogba amesema alikuwa anataraji kushinda taji hilo la Ligi ya Mabingwa Ulaya, akiita ” Tji nililolikiria, mimi daima liko katika akili yangu.”

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents