Michezo

Pogba afeli usajili kutokana na minyama uzembe

Wakati klabu kubwa duniani zikihaha kuwania saini ya kiungo wa Manchester United, Paul Pogba hali hiyo ni tofauti na kwa kaka yake ambaye inapata mwaka sasa amekosa timu ya kuitumikia.

 

Mathias Pogba mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni kaka mkubwa wa Paul Pogba ameshindwa kujiunga na klabu ya KFC Uerdingen ya nchini Ujerumani baada ya kufeli majaribio kutokana na kuwa na mwili mkubwa unaochangia kumjengea kuwa na hips na ongezeko la kilo.

Alipohojiwa kuhusu kushindwa kujiunga na KFC Uerdingen Meneja wa klabu hiyo, Stefan Kramer amesema Pogba tayari ameshaondoka baada ya kufeli majaribio.

Pogba tayari ameshaondoka, hawezi kuisaidia timu yetu. Bado hajakuwa kwenye shepu nzuri ya kimazoezi licha ya kuwa na mwili mkubwa kwa namba nane lakini bado ana kilo nyingi.

Mathias Pogba mwenye umbile kubwa la futi 6 anayeitumikia timu ya taifa ya Guinea kwa sasa ni mchezaji huru toka kuacha kuitumikia klabu ya Sparta Rotterdam mwaka 2017 hana timu.

Mathias (kulia) mdogo ake Paul (katikati) na ndugu yao Florentin (kushoto) wakisherehekea ubingwa wa kombe la dunia baada ya Ufaransa kutwaa nchini Urusi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents